«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 93

1  Bwana ametamalaki, amejivika adhama, Bwana amejivika, na kujikaza nguvu. Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;

2  Kiti chako kimekuwa thabiti tokea zamani; Wewe ndiwe uliye tangu milele.

3  Ee Bwana, mito imepaza, Mito imepaza sauti zake, Mito imepaza uvumi wake.

4  Kupita sauti ya maji mengi, maji makuu, Kupita mawimbi ya bahari yaumkayo, Bwana Aliye juu ndiye mwenye ukuu.

5  Shuhuda zako ni amini sana; Utakatifu ndio uifaao nyumba yako, Ee Bwana, milele na milele.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23