«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 87

1  Msingi wake upo Juu ya milima mitakatifu.

2  Bwana ayapenda malango ya Sayuni Kuliko maskani zote za Yakobo.

3  Umetajwa kwa mambo matukufu, Ee Mji wa Mungu.

4  Nitataja Rahabu na Babeli Miongoni mwao wanaonijua. Tazama Filisti, na Tiro, na Kushi; Huyu alizaliwa humo.

5  Naam, mintarafu Sayuni itasemwa, Huyu na huyu alizaliwa humo. Na Yeye Aliye juu Ataufanya imara.

6  Bwana atahesabu, awaandikapo mataifa, Huyu alizaliwa humo.

7  Waimbao na wachezao na waseme, Visima vyangu vyote vimo mwako.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23