«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 82

1  Mungu asimama katika kusanyiko la Mungu; Katikati ya miungu anahukumu.

2  Hata lini mtahukumu kwa dhuluma, Na kuzikubali nyuso za wabaya?

3  Mfanyieni hukumu maskini na yatima; Mtendeeni haki aliyeonewa na fukara;

4  Mwokoeni maskini na mhitaji; Mwopoeni mikononi mwa wadhalimu.

5  Hawajui wala hawafahamu, hutembea gizani; Misingi yote ya nchi imetikisika.

6  Mimi nimesema, Ndinyi miungu, Na wana wa Aliye juu, nyote pia.

7  Lakini mtakufa kama wanadamu, Mtaanguka kama mmoja wa wakuu.

8  Ee Mungu, usimame, uihukumu nchi, Maana Wewe utawarithi mataifa yote.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23