«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 8

1  Wewe, MUNGU, Bwana wetu Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote! Wewe umeuweka utukufu wako mbinguni;

2  Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao Umeiweka misingi ya nguvu; Kwa sababu yao wanaoshindana nawe; Uwakomeshe adui na mijilipiza kisasi.

3  Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, Mwezi na nyota ulizoziratibisha;

4  Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie?

5  Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima;

6  Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.

7  Kondoo, na ng'ombe wote pia; Naam, na wanyama wa kondeni;

8  Ndege wa angani, na samaki wa baharini; Na kila kipitacho njia za baharini.

9  Wewe, MUNGU, Bwana wetu, Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23