«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 75

1  Ee Mungu, twakushukuru. Twakushukuru kwa kuwa Jina lako li karibu; Watu huyasimulia matendo yako ya ajabu.

2  Nitakapoufikia wakati ulioamriwa, Mimi nitahukumu hukumu za haki.

3  Ingawa dunia na wote wakaao humo wataharuki, Mimi mwenyewe nimezisimamisha nguzo zake.

4  Naliwaambia waliojivuna, Msijivune; Na wasio haki, Msiiinue pembe.

5  Msiiinue pembe yenu juu, Wala msinene kwa shingo ya kiburi.

6  Maana siko mashariki wala magharibi, Wala nyikani itokako heshima.

7  Bali Mungu ndiye ahukumuye; Humdhili huyu na kumwinua huyu.

8  Maana mkononi mwa Bwana mna kikombe, Na mvinyo yake inatoka povu; Kumejaa machanganyiko; Naye huyamimina. Na sira zake wasio haki wa dunia Watazifyonza na kuzinywa.

9  Bali mimi nitatangaza matendo yako milele, Nitamwimbia Mungu wa Yakobo.

10  Pembe zote za wasio haki nitazikata, Na pembe za mwenye haki zitainuka.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23