«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 70

1  Ee Mungu, uniokoe, Ee Bwana, unisaidie hima.

2  Waaibike, wafedheheke, Wanaoitafuta nafsi yangu. Warudishwe nyuma, watahayarishwe, Wapendezwao na shari yangu.

3  Warudi nyuma, na iwe aibu yao, Wanaosema, Ewe! Ewe!

4  Washangilie, wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima, Atukuzwe Mungu.

5  Nami ni maskini na mhitaji, Ee Mungu, unijilie kwa haraka. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu, Ee Bwana, usikawie.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23