«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 67

1  Mungu na atufadhili na kutubariki, Na kutuangazia uso wake.

2  Njia yake ijulike duniani, Wokovu wake katikati ya mataifa yote.

3  Watu na wakushukuru, Ee Mungu, Watu wote na wakushukuru.

4  Mataifa na washangilie, Naam, waimbe kwa furaha, Maana kwa haki utawahukumu watu, Na kuwaongoza mataifa walioko duniani.

5  Watu na wakushukuru, Ee Mungu, Watu wote na wakushukuru.

6  Nchi imetoa mazao yake MUNGU, Mungu wetu, ametubariki.

7  Mungu atatubariki sisi; Miisho yote ya dunia itamcha Yeye.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23