«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 56

1  Mungu, unirehemu, maana yuko atakaye kunimeza, Mchana kutwa ananionea akileta vita.

2  Adui zangu wanataka kunimeza mchana kutwa, Maana waletao vita juu yangu kwa kiburi ni wengi.

3  Siku ya hofu yangu nitakutumaini Wewe;

4  Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake. Nimemtumaini Mungu, sitaogopa; Mwenye mwili atanitenda nini?

5  Mchana kutwa wanapotosha maneno yangu, Mawazo yao yote ni juu yangu kunitakia mabaya.

6  Hukutanika, hujificha, huziangalia nyayo zangu, Kwa kuwa wameniotea nafsi yangu.

7  Je! Wataokoka kwa uovu wao? Ee Mungu, uwaangamize kwa hasira yako.

8  Umehesabu kutanga-tanga kwangu; Uyatie machozi yangu katika chupa yako; (Je! Hayamo katika kitabu chako?)

9  Ndipo adui zangu watarudi nyuma siku ile niitapo. Neno hili najua kuwa MUNGU yu upande wangu;

10  Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake. Kwa msaada wa Bwana nitalisifu neno lake.

11  Nimemtumaini Mungu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?

12  Ee Mungu, nadhiri zako zi juu yangu; Nitakutolea dhabihu za kushukuru.

13  Maana umeniponya nafsi yangu na mauti; Je! Hukuizuia miguu yangu isianguke? Ili nienende mbele za Mungu Katika nuru ya walio hai.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23