«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 52

1  Kwa nini kujisifia uovu, Ewe jabari? Wema wa Mungu upo sikuzote.

2  Ulimi wako watunga madhara, Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila

3  Umependa mabaya kuliko mema, Na uongo kuliko kusema kweli.

4  Umependa maneno yote ya kupoteza watu, Ewe ulimi wenye hila.

5  Lakini Mungu atakuharibu hata milele; Atakuondolea mbali; Atakunyakua hemani mwako; Atakung'oa katika nchi ya walio hai.

6  Nao wenye haki wataona; Wataingiwa na hofu na kumcheka;

7  Kumbe! Huyu ndiye mtu yule, Asiyemfanya Mungu kuwa nguvu zake. Aliutumainia wingi wa mali zake, Na kujifanya hodari kwa madhara yake.

8  Bali mimi ni kama mzeituni Umeao katika nyumba ya Mungu. Nazitumainia fadhili za Mungu milele na milele.

9  Nitakushukuru milele kwa maana umetenda; Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema; Mbele ya wacha Mungu wako.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23