«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 4

1  Ee Mungu wa haki yangu, uniitikie niitapo; Umenifanyizia nafasi wakati wa shida; Unifadhili na kuisikia sala yangu.

2  Enyi wanadamu, hata lini utukufu wangu utafedheheka? Je! Mtapenda ubatili na kutafuta uongo?

3  Bali jueni ya kuwa Bwana amejiteulia mtauwa; Bwana atasikia nimwitapo.

4  Mwe na hofu wala msitende dhambi, Tafakarini vitandani mwenu na kutulia.

5  Toeni dhabihu za haki, Na kumtumaini Bwana.

6  Wengi husema, Nani atakayetuonyesha mema? Bwana, utuinulie nuru ya uso wako.

7  Umenitia furaha moyoni mwangu, Kupita yao wanapozidishiwa nafaka na divai.

8  Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara, Maana Wewe, Bwana, peke yako, Ndiwe unijaliaye kukaa salama.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23