«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 3

1  Bwana, watesi wangu wamezidi kuwa wengi, Ni wengi wanaonishambulia,

2  Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu, Hana wokovu huyu kwa Mungu.

3  Na Wewe, Bwana, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu na mwinua kichwa changu.

4  Kwa sauti yangu namwita Bwana Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu.

5  Nalijilaza nikalala usingizi, nikaamka, Kwa kuwa Bwana ananitegemeza.

6  Sitayaogopa makumi elfu ya watu, Waliojipanga juu yangu pande zote.

7  Bwana, uinuke, Mungu wangu, uniokoe, Maana umewapiga taya adui zangu wote; Umewavunja meno wasio haki.

8  Wokovu una Bwana; Baraka yako na iwe juu ya watu wako.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23