«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 20

1  Bwana akujibu siku ya dhiki, Jina la Mungu wa Yakobo likuinue.

2  Akupelekee msaada toka patakatifu pake, Na kukutegemeza toka Sayuni.

3  Azikumbuke sadaka zako zote, Na kuzitakabali dhabihu zako.

4  Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, Na kuyatimiza mashauri yako yote.

5  Na tuushangilie wokovu wako, Kwa jina la Mungu wetu tuzitweke bendera zetu. Bwana akutimizie matakwa yako yote.

6  Sasa najua kuwa Bwana amwokoa masihi

7  Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja jina la Bwana, Mungu wetu.

8  Wao wameinama na kuanguka, Bali sisi tumeinuka na kusimama.

9  Bwana, umwokoe mfalme, Utuitikie siku tuitayo.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23