«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 150

1  Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake.

2  Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.

3  Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi;

4  Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi;

5  Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana.

6  Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. Haleluya.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23