«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 149

1  Haleluya. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Sifa zake katika kusanyiko la watauwa.

2  Israeli na amfurahie Yeye aliyemfanya, Wana wa Sayuni na wamshangilie mfalme wao.

3  Na walisifu jina lake kwa kucheza, Kwa matari na kinubi wamwimbie.

4  Kwa kuwa Bwana awaridhia watu wake, Huwapamba wenye upole kwa wokovu.

5  Watauwa na waushangilie utukufu, Waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao.

6  Sifa kuu za Mungu na ziwe vinywani mwao, Na upanga mkali kuwili mikononi mwao.

7  Ili kufanya kisasi juu ya mataifa, Na adhabu juu ya kabila za watu.

8  Wawafunge wafalme wao kwa minyororo, Na wakuu wao kwa pingu za chuma.

9  Kuwafanyia hukumu iliyoandikwa; Hiyo ndiyo heshima ya watauwa wake wote. Haleluya.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23