«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 142

1  Kwa sauti yangu nitamlilia Bwana, Kwa sauti yangu nitamwomba Bwana dua.

2  Nitafunua mbele zake malalamiko yangu, Shida yangu nitaitangaza mbele zake.

3  Nilipozimia roho uliyajua mapito yangu; Katika njia niendayo wamenifichia mtego.

4  Utazame mkono wa kuume ukaone, Kwa maana sina mtu anijuaye. Makimbilio yamenipotea, Hakuna wa kunitunza roho.

5  Bwana, nimekuita nikasema, Ndiwe kimbilio langu, Fungu langu katika nchi ya walio hai.

6  Ukisikilize kilio changu, Kwa maana nimedhilika sana. Uniponye nao wanaonifuatia, Kwa maana wao ni hodari kuliko mimi.

7  Uitoe nafsi yangu kifungoni. Nipate kulishukuru jina lako. Wenye haki watanizunguka, Kwa kuwa Wewe unanikirimu.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23