«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 141

1  Ee Bwana, nimekuita, unijie hima, Uisikie sauti yangu nikuitapo.

2  Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba, Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni.

3  Ee Bwana, uweke mlinzi kinywani pangu, Mngojezi mlangoni pa midomo yangu.

4  Usiuelekeze moyo wangu kunako jambo baya, Nisiyazoelee matendo yasiyofaa, Pamoja na watu watendao maovu; Wala nisile vyakula vyao vya anasa.

5  Mwenye haki na anipige, itakuwa fadhili; Anikemee, itakuwa kama mafuta kichwani; Kichwa changu kisikatae, Maana siachi kusali kati ya mabaya yao.

6  Makadhi wao wakiangushwa kando ya genge, Watayasikia maneno yangu, maana ni matamu.

7  Kama kupasua kuni na kuzichanja juu ya nchi, Ndivyo ilivyo mifupa yetu mdomoni pa kuzimu.

8  Macho yangu yanakuelekea Wewe, MUNGU Bwana, Nimekukimbilia Wewe, usiniache nafsi yangu.

9  Unilinde na mtego walionitegea, Na matanzi yao watendao maovu.

10  Wabaya na waanguke katika nyavu zao wenyewe, Pindi mimi ninapopita salama.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23