«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 137

1  Kando ya mito ya Babeli ndiko tulikoketi, Tukalia tulipoikumbuka Sayuni.

2  Katika miti iliyo katikati yake Tulivitundika vinubi vyetu.

3  Maana huko waliotuchukua mateka Walitaka tuwaimbie; Na waliotuonea walitaka furaha; Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni.

4  Tuuimbeje wimbo wa Bwana Katika nchi ya ugeni?

5  Ee Yerusalemu, nikikusahau wewe, Mkono wangu wa kuume na usahau.

6  Ulimi wangu na ugandamane Na kaakaa la kinywa changu, nisipokukumbuka. Nisipoikuza Yerusalemu Zaidi ya furaha yangu iliyo kuu.

7  Ee Bwana, uwakumbuke wana wa Edomu, Siku ya Yerusalemu. Waliosema, Bomoeni! Bomoeni hata misingini!

8  Ee binti Babeli, uliye karibu na kuangamia, Heri atakayekupatiliza, ulivyotupatiliza sisi.

9  Heri yeye atakayewakamata wadogo wako, Na kuwaseta wao juu ya mwamba.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23