«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 136

1  Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

2  Mshukuruni Mungu wa miungu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

3  Mshukuruni Bwana wa mabwana; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

4  Yeye peke yake afanya maajabu makuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

5  Yeye aliyefanya mbingu kwa fahamu zake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

6  Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

7  Yeye aliyefanya mianga mikubwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

8  Jua litawale mchana; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

9  Mwezi na nyota zitawale usiku; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

10  Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wa kwanza wao; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

11  Akawatoa Waisraeli katikati yao; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

12  Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

13  Yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

14  Akawavusha Israeli katikati yake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

15  Akamwangusha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

16  Yeye aliyewaongoza watu wake jangwani; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

17  Yeye aliyewapiga wafalme wakuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

18  Akawaua wafalme mashuhuri; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

19  Sihoni, mfalme wa Waamori; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

20  Na Ogu, mfalme wa Bashani; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

21  Akaitoa nchi yao iwe urithi; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

22  Urithi wa Israeli mtumishi wake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

23  Aliyetukumbuka katika unyonge wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

24  Akatuokoa na watesi wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

25  Kila chenye mwili akipa chakula chake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

26  Mshukuruni Mungu wa mbingu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23