«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 133

1  Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, Ndugu wakae pamoja, kwa umoja.

2  Ni kama mafuta mazuri kichwani, Yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni, Yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake.

3  Kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni. Maana ndiko Bwana alikoamuru baraka, Naam, uzima hata milele.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23