«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 130

1  Ee Bwana, toka vilindini nimekulilia.

2  Bwana, uisikie sauti yangu. Masikio yako na yaisikilize Sauti ya dua zangu.

3  Bwana, kama Wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama?

4  Lakini kwako kuna msamaha, Ili Wewe uogopwe.

5  Nimemngoja Bwana, roho yangu imengoja, Na neno lake nimelitumainia.

6  Nafsi yangu inamngoja Bwana, Kuliko walinzi waingojavyo asubuhi, Naam, walinzi waingojao asubuhi.

7  Ee Israeli, umtarajie Bwana; Maana kwa Bwana kuna fadhili, Na kwake kuna ukombozi mwingi.

8  Yeye atamkomboa Israeli na maovu yake yote.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23