«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 13

1  Ee Bwana, hata lini utanisahau, hata milele? Hata lini utanificha uso wako?

2  Hata lini nifanye mashauri nafsini mwangu, Nikihuzunika moyoni mchana kutwa? Hata lini adui yangu atukuke juu yangu?

3  Ee Bwana, Mungu wangu, uangalie, uniitikie; Uyatie nuru macho yangu, Nisije nikalala usingizi wa mauti.

4  Adui yangu asije akasema, Nimemshinda; Watesi wangu wasifurahi ninapoondoshwa.

5  Nami nimezitumainia fadhili zako; Moyo wangu na uufurahie wokovu wako.

6  Naam, nimwimbie Bwana, Kwa kuwa amenitendea kwa ukarimu.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23