«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 129

1  Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu, Israeli na aseme sasa,

2  Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu, Lakini hawakuniweza.

3  Wakulima wamelima mgongoni mwangu, Wamefanya mirefu mifuo yao.

4  Bwana ndiye mwenye haki, Amezikata kamba zao wasio haki.

5  Na waaibishwe, warudishwe nyuma, Wote wanaoichukia Sayuni.

6  Na wawe kama majani ya darini Yanyaukayo kabla hayajamea.

7  Ambayo mvunaji haujazi mkono wake, Wala mfunga miganda kifua chake.

8  Wala hawasemi wapitao, Amani ya Bwana ikae nanyi, Twawabariki kwa jina la Bwana.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23