«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 128

1  Heri kila mtu amchaye Bwana, Aendaye katika njia yake.

2  Taabu ya mikono yako hakika utaila; Utakuwa heri, na kwako kwema.

3  Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao, Vyumbani mwa nyumba yako. Wanao kama miche ya mizeituni Wakiizunguka meza yako.

4  Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye Bwana.

5  Bwana akubariki toka Sayuni; Uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako;

6  Naam, ukawaone wana wa wanao. Amani ikae na Israeli.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23