«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 126

1  Bwana alipowarejeza mateka wa Sayuni, Tulikuwa kama waotao ndoto.

2  Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko, Na ulimi wetu kelele za furaha. Ndipo waliposema katika mataifa, Bwana amewatendea mambo makuu.

3  Bwana alitutendea mambo makuu, Tulikuwa tukifurahi.

4  Ee Bwana, uwarejeze watu wetu waliofungwa, Kama vijito vya Kusini.

5  Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha.

6  Ingawa mtu anakwenda zake akilia, Azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha, Aichukuapo miganda yake.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23