«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 125

1  Wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele.

2  Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele.

3  Kwa maana fimbo ya udhalimu Haitakaa juu ya fungu la wenye haki; Wenye haki wasije wakainyosha Mikono yao kwenye upotovu.

4  Ee Bwana, uwatendee mema walio wema, Nao walio wanyofu wa moyo.

5  Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka, Bwana atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani ikae na Israeli.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23