«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 124

1  Kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi, Israeli na aseme sasa,

2  Kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi, Wanadamu walipotushambulia.

3  Papo hapo wangalitumeza hai, Hasira yao ilipowaka juu yetu

4  Papo hapo maji yangalitugharikisha, Mto ungalipita juu ya roho zetu;

5  Papo hapo yangalipita juu ya nafsi zetu Maji yafurikayo.

6  Na ahimidiwe Bwana; Asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno yao.

7  Nafsi yetu imeokoka kama ndege Katika mtego wa wawindaji, Mtego umevunjika, nasi tumeokoka.

8  Msaada wetu u katika jina la Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23