«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 123

1  Nimekuinulia macho yangu, Wewe uketiye mbinguni.

2  Kama vile macho ya watumishi Kwa mkono wa bwana zao Kama macho ya mjakazi Kwa mkono wa bibi yake; Hivyo macho yetu humwelekea Bwana, Mungu wetu, Hata atakapoturehemu.

3  Uturehemu, Ee Bwana, uturehemu sisi, Kwa maana tumeshiba dharau.

4  Nafsi zetu zimeshiba mzaha wa wenye raha, Na dharau ya wenye kiburi.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23