«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 122

1  Nalifurahi waliponiambia, Na twende nyumbani kwa Bwana.

2  Miguu yetu imesimama Ndani ya malango yako, Ee Yerusalemu.

3  Ee Yerusalemu uliyejengwa Kama mji ulioshikamana,

4  Huko ndiko walikopanda kabila, Kabila za Bwana; Ushuhuda kwa Israeli, Walishukuru jina la Bwana.

5  Maana huko viliwekwa viti vya hukumu, Viti vya enzi vya mbari ya Daudi.

6  Utakieni Yerusalemu amani; Na wafanikiwe wakupendao;

7  Amani na ikae ndani ya kuta zako, Na kufanikiwa ndani ya majumba yako.

8  Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu Niseme sasa, Amani ikae nawe.

9  Kwa ajili ya nyumba ya Bwana, Mungu wetu, Nikutafutie mema.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23