«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 121

1  Nitayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi?

2  Msaada wangu u katika Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi.

3  Asiuache mguu wako usogezwe; Asisinzie akulindaye;

4  Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli.

5  Bwana ndiye mlinzi wako; Bwana ni uvuli mkono wako wa kuume.

6  Jua halitakupiga mchana, Wala mwezi wakati wa usiku.

7  Bwana atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako.

8  Bwana atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23