«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 120

1  Katika shida yangu nalimlilia Bwana Naye akaniitikia.

2  Ee Bwana, uiponye nafsi yangu Na midomo ya uongo na ulimi wa hila.

3  Akupe nini, akuzidishie nini, Ewe ulimi wenye hila?

4  Mishale ya mtu hodari iliyochongoka, Pamoja na makaa ya mretemu.

5  Ole wangu mimi! Kwa kuwa nimekaa katika Mesheki; Na kufanya maskani yangu Katikati ya hema za Kedari.

6  Nafsi yangu imekaa siku nyingi, Pamoja naye aichukiaye amani.

7  Mimi ni wa amani; Bali ninenapo, wao huelekea vita.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23