«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 114

1  Haleluya. Israeli alipotoka Misri, Na Yakobo katika watu wa lugha ya kigeni.

2  Yuda ilikuwa patakatifu pake, Israeli milki yake.

3  Bahari iliona ikakimbia, Yordani ilirudishwa nyuma.

4  Milima iliruka kama kondoo waume, Vilima kama wana-kondoo.

5  Ee bahari, una nini, ukimbie? Yordani, urudi nyuma?

6  Enyi milima, mruke kama kondoo waume? Enyi vilima, kama wana-kondoo?

7  Tetemeka, Ee nchi, mbele za uso wa Bwana, Mbele za uso wa Mungu wa Yakobo.

8  Augeuza mwamba kuwa ziwa la maji, Jiwe gumu kuwa chemchemi.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23