«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 112

1  Haleluya. Heri mtu yule amchaye Bwana, Apendezwaye sana na maagizo yake.

2  Wazao wake watakuwa hodari duniani; Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa.

3  Nyumbani mwake mna utajiri na mali, Na haki yake yakaa milele.

4  Nuru huwazukia wenye adili gizani; Ana fadhili na huruma na haki.

5  Heri atendaye fadhili na kukopesha; Atengenezaye mambo yake kwa haki.

6  Kwa maana hataondoshwa kamwe; Mwenye haki atakumbukwa milele.

7  Hataogopa habari mbaya; Moyo wake u imara ukimtumaini Bwana.

8  Moyo wake umethibitika hataogopa, Hata awaone watesi wake wameshindwa.

9  Amekirimu, na kuwapa maskini, Haki yake yakaa milele, Pembe yake itatukuzwa kwa utukufu.

10  Asiye haki ataona na kusikitika, Atasaga meno yake na kuyeyuka, Tamaa ya wasio haki itapotea.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23