«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 100

1  Mfanyieni Bwana shangwe, dunia yote;

2  Mtumikieni Bwana kwa furaha; Njoni mbele zake kwa kuimba;

3  Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu; Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake; Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.

4  Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake;

5  Kwa kuwa Bwana ndiye mwema; Rehema zake ni za milele; Na uaminifu wake vizazi na vizazi.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23