«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Zaburi 1

1  Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.

2  Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.

3  Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.

4  Sivyo walivyo wasio haki; Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.

5  Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni, Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki.

6  Kwa kuwa Bwana anaijua njia ya wenye haki, Bali njia ya wasio haki itapotea.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23