«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Ayubu 25

1  Ndipo Bildadi, Mshuhi, akajibu, na kusema,

2  Enzi na hofu zi pamoja naye; Hufanya amani katika mahali pake palipoinuka.

3  Je! Majeshi yake yahesabika? Ni nani asiyetokewa na mwanga wake?

4  Basi mtu awezaje kuwa na haki mbele ya Mungu? Au awezaje kuwa safi aliyezaliwa na mwanamke?

5  Tazama, hata mwezi hauangazi, Wala nyota si safi machoni pake;

6  Siuze mtu, aliye mdudu! Na mwanadamu, ambaye ni buu!

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23