«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Ayubu 23

1  Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,

2  Hata leo mashitaka yangu yana uchungu; Pigo langu ni zito zaidi ya kuugua kwangu.

3  Laiti ningejua mahali niwezapo kumwona, Nifike hata hapo anapokaa!

4  Ningeiweka daawa yangu mbele yake, Na kukijaza kinywa changu hoja.

5  Ningeyajua maneno atakayonijibu, Na kuelewa na hayo atakayoniambia.

6  Je! Angeshindana nami kwa ukuu wa uwezo wake? La, lakini angenisikiliza.

7  Hapo walekevu wangepata kuhojiana naye; Basi hivyo ningeachiliwa na mwamuzi wangu milele.

8  Tazama, naenda mbele, wala hayuko; Narudi nyuma, lakini siwezi kumwona;

9  Na mkono wa kushoto, afanyapo kazi, lakini siwezi kumwona; Hujificha upande wa kuume, hata nisimwone.

10  Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.

11  Mguu wangu umeshikamana sana na hatua zake; Njia yake nimeishika, wala sikukengeuka.

12  Sikurudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake; Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu,

13  Lakini yeye ni mmoja, ni nani awezaye kumgeuza? Tena nafsi yake ilitakalo, ndilo afanyalo.

14  Kwani yeye hulitimiliza hilo nililoamuriwa; Tena mambo mengi kama hayo ya pamoja naye.

15  Kwa hiyo naona taabu mbele ya uso wake; Nitakapofikiri, namwogopa.

16  Kwani Mungu ameufanya moyo wangu kuzimia, Naye Mwenyezi amenitaabisha;

17  Maana sikufadhaishwa kwa sababu ya giza, Wala kwa sababu giza kuu limenifunika uso.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23