«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

Mwanzo 9

1  Mungu akambariki Nuhu na wanawe, akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi.

2  Kila mnyama wa katika nchi atawaogopa ninyi na kuwahofu, na kila ndege wa angani: pamoja na vitu vyote vilivyojaa katika ardhi, na samaki wote wa baharini; vimetiwa mikononi mwenu.

3  Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote.

4  Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile.

5  Hakika damu yenu ya uhai wenu nitaitaka; na kwa mkono wa kila mnyama nitaitaka; na kwa mkono wa mwanadamu, kwa mkono wa ndugu ya mtu nitataka uhai wa mwanadamu.

6  Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu, maana kwa mfano wake Mungu alimfanya mwanadamu.

7  Nanyi zaeni, mkaongezeke; zaeni sana katika nchi, mkaongezeke ndani yake.

8  Mungu akamwambia Nuhu, na wanawe pamoja naye, akisema,

9  Mimi, tazama, nalithibitisha agano langu nanyi; tena na uzao wenu baada yenu;

10  tena na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, ndege, na mnyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu katika nchi pamoja nanyi; wote wanaotoka katika safina, hata kila kilicho hai katika nchi.

11  Na agano langu nitalithibitisha nanyi; wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika; wala hakutakuwa tena gharika, baada ya hayo, kuiharibu nchi.

12  Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano nifanyalo kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, kwa vizazi vyote hata milele;

13  Mimi nauweka upinde wangu winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi.

14  Hata itakuwa nikitanda mawingu juu ya nchi, upinde utaonekana winguni,

15  nami nitalikumbuka agano langu, lililoko kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili, wala maji hayatakuwa gharika tena kuwaharibu wote wenye mwili.

16  Basi huo upinde utakuwa winguni; nami nitauangalia nipate kulikumbuka agano la milele lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili kilichoko katika nchi.

17  Mungu akamwambia Nuhu, Hii ndiyo ishara ya agano nililoliweka kati yangu na wote wenye mwili walioko katika nchi.

18  Wana wa Nuhu waliotoka katika safina, ni Shemu, na Hamu, na Yafethi; na Hamu ndiye baba wa Kanaani.

19  Hawa watatu walikuwa wana wa Nuhu na kwa hao nchi yote ikaenea watu.

20  Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu;

21  akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.

22  Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.

23  Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao.

24  Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea.

25  Akasema,

26  Akasema,

27  Mungu akamnafisishe Yafethi.

28  Na Nuhu akaishi baada ya ile gharika miaka mia tatu na hamsini.

29  Siku zote za Nuhu zilikuwa miaka mia kenda na hamsini, akafa.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23