«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »

1 Mambo ya Nyakati 25

1  Tena Daudi na maakida wa jeshi wakatenga kwa utumishi baadhi ya wana wa Asafu, na wa Hemani, na wa Yeduthuni, watakaotabiri kwa vinubi na vinanda, na matoazi; hii ndiyo hesabu ya wafanya kazi sawasawa na utumishi wao;

2  wa wana wa Asafu; Zakuri, na Yusufu, na Nethania, na Asharela, wana wa Asafu; walioamriwa na Asafu, aliyetabiri kwa amri ya mfalme.

3  Wa Yeduthuni; wana wa Yeduthuni; Gedalia, na Seri, na Yeshaya, na Hashabia, na Matithia, [na Shimei], watu sita; walioamriwa na baba yao Yeduthuni mwenye kinubi, aliyetabiri katika kumshukuru na kumsifu Bwana.

4  Wa Hemani; wana wa Hemani; Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli, na Yeremothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti, na Romanti-ezeri, Yoshbekasha, Malothi, Hothiri, Mahaziothi;

5  hao wote ndio wana wa Hemani, mwonaji wa mfalme, kwa maneno ya Mungu, ili kuinua pembe. Naye Mungu akampa Hemani wana kumi na wanne na binti watatu.

6  Hao wote waliamriwa na baba yao, waimbe nyumbani mwa Bwana, wakiwa na matoazi, vinanda, na vinubi, kwa utumishi wa nyumba ya Mungu; Asafu, Yeduthuni, na Hemani wakiwa wanaamriwa na mfalme.

7  Na hesabu yao, pamoja na ndugu zao waliofundishwa kumwimbia Bwana, wote waliokuwa wastadi, walikuwa mia mbili na themanini na wanane.

8  Wakatupiwa kura ya ulinzi wao, sawasawa wote, mdogo kwa mkubwa, mwalimu kwa mwanafunzi.

9  Kura ya kwanza ikamtokea Yusufu, kwa Asafu; ya pili Gedalia; yeye na nduguze na wanawe, kumi na wawili;

10  ya tatu Zakuri, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

11  ya nne Seri, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

12  ya tano Nethania, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

13  ya sita Bukia, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

14  ya saba Asharela, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

15  ya nane Yeshaya, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

16  ya kenda Matania wanawe na nduguze, kumi na wawili;

17  ya kumi Shimei, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

18  ya kumi na moja Uzieli, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

19  ya kumi na mbili Hashabia, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

20  ya kumi na tatu Shebueli, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

21  ya kumi na nne Matithia, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

22  ya kumi na tano Yeremothi, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

23  ya kumi na sita Hanania, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

24  ya kumi na saba Yoshbekasha, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

25  ya kumi na nane Hanani, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

26  ya kumi na kenda Malothi, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

27  ya ishirini Eliatha, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

28  ya ishirini na moja Hothiri, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

29  ya ishirini na mbili Gidalti, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

30  ya ishirini na tatu Mahaziothi, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

31  ya ishirini na nne Romanti-ezeri, wanawe na nduguze, kumi na wawili.

«  Sura ijayo   |   Chagua sura   |   Kitabu kijacho  »
“Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.” — 1 Wakorintho 16:23